Makanisa mengi karibu yote huonyesha na kuanika yote wazi msalaba maana katika Imani na mafundisho ya ukristo msalaba ni lazima. Warumi walitumia msalba kuwatesa na kuhukumu waasi. Sisi wakristo huzingatia na kuhimiza ujumbe na somo la msalaba. Somo na ujumbe wa kuteswa kwake bwana wetu yesu kristo msalabani kwa sababu ya makossa na dhambi zetu. Ilikuwa muhimu kristo afe msalabani kwaajili na kwasabau yetu sisi wenye dhambi
Katika maisha yetu tunavyo vitu tunavyothamini kuliko vingine kulingana na umuhimu wa vitu vile katika maisha yetu. Hii ni baada ya uchunguzi na upelelezi wa kina sana na hivyo basi mtu aweza kuwa na Imani na kile chombo au kituLakini hapa Paulo atufunza Imani ilivyo maana Zaidi